Sunday, September 30, 2012

CHEKA AMKATA NGEBE NYINAWILA.

Francis Cheka jana alimuonesha mpinzani wake bondia Karama  Nyilawila kwenye ukumbi wa PTA baada ya kushinda kwa K.O.
Kabla ya mpambano huo Nyilawila alisema atamuonesha Cheka baada ya kudai kua anapendelewa na majaji hasa kwa mpambano alioshinda morogoro kwa point dhidi yake,Upande wa Cheka hakuongea sana ila alisema ''mkono'' ndo utaongea na ndicho alikifanya kwenye mpambano huo.
Bondia huyo kutoka mji kasoro bahari'city without ocean' alifurahi sana kwa kumkata kauli mpinzani wake ipasavyo baada ya kushindwa kuendelea na mpambano kutoka na ngumi nzito alizomtupia.
Baadhi ya picha za tukio hilo la jana ni hizi zifuatazo:
Cheka na Nyinawila wakitupiana makonde.
Cheka akimtwanga konde zito mpinzani wake.
Nyinawila akiwa chini baada ya kushindwa kustahimili konde kutoka kwa Cheka.
Nyinawila akisema 'mie basi' huku Cheka akizuiwa na Mwamuzi.
Mwana-moro akishangilia baada ya Nyinawila kkushindwa kuendelea na pambano.
Mashabiki wakiwa makini kwenye pambano hilo
Afande Kova ambaye ni mlezi wa ngumi Tanzania akijiandaa kumvalisha Cheka mkanda.
Bondia Fransis Cheka hadi sasa ndiye bondia anayeongoza Tz baada ya kuwapiga mabondia wengi na kuonekana amekosa mpinzani nchini.


                                                            picha kutoka:''sportseyetz.blogspot.com''

No comments:

Post a Comment