Washika bunduki wa london Arsenal leo wamekubali kipigo kutoka kwa mabingwa wa Ulaya Chelsea kwa kukubali kipigo cha bao 2-1 mbele ya mashabiki wao.
Chelsea walikua wakwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake Fernand Torres dk ya 20 kutokana na mpira wa adhabu uliosababishwa na nahodha Thomas Vermaleen iliyopigwa na Mata.
|
Torres akifunga goli la kwanza dhidi ya Arsenal. |
|
|
Torres akishangilia bao alilofunga mbele ya nahodha John Terry. |
|
Ikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mapumziko,Arsenal walisawazisha goli kupitia kwa winga wake raia wa Ivory Coast Gervinho katika dakika ya 42 ya mchezo na kufanya matokeo yawe 1-1 hadi wanaenda mapumziko.
|
Gervinho akisawazisha goli katika dakika 42 ya mchezo. |
|
Gervinho akishangilia na Chamberlain |
C helsea hawakuishia hapo,waliongeza goli la pili kupia kwa mchezaji wake Mata katika dakika 52 ya mchezo.
|
mfungaji wa goli la pili la chelsea,Mata. |
Kwa ushindi huo Chelsea wanaongoza ligi kwa kuwa na pointi 16 mkononi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwa michezo sita ya hadi sasa.
ARSENAL HAIKUPOYEZA MECHI HATA MOJA KATIKA MECHI TANO ZILIZOPITA TOKA MSIMU UANZE AMBAPO KICHAPO CHA LEO NDO KIMEONDOA HISTORIA HIYO FUPI YA MDA.
No comments:
Post a Comment