Kocha wa timu ya Manchester City ya nchini Uingereza,Roberto Mancini amesema anauhakika siku moja timu yake itachukua kombe la klabu bingwa ulaya japo hana uhakika itakua lini.Kocha huyo ambaye ni raia wa Italia amesema kutokana na mipango ya timu hiyo na hali ya wachezaji ambayo unakua kila siku kuna uwezekano mkubwa sana wa kulichukua kombe hilo.
Manchester city iliingia katika mashindano hayo makubwa kwa mara ya kwanza msimu uliopita ambapo haikufanya vizuri.Msimu huu timu hiyo imeingia tena katika mashindano hayo huku ikiwa imepengwa katika kundi linaloonekana kama ni gumu sna"kundi la kifo" wakiwa pamoja na mabingwa wa hispania msimu uliopita Real Madrid.
Man City inaanza kutupa karata yake leo katika michuano hiyo ya Ulaya ikiikabili timu ngumu ya real Madrid.
Swali ni kwamba Mancini anaona uwezekano wa kuchukua kombe hilo msimu huu ni ngumu au anawapumbaza wapinzani wao Madrid katika mchezo wa leo?
No comments:
Post a Comment