Texan Mayra Rosales mwenye uzito wa kg 1,100 ambaye alidanganya mahakamani ameua ili kumlinda dada ake aliyehusika na kitendo hicho.
Mayra alisema anastahili kuadhibiwa kutokana na kitendo alichofanya wakati akikiri mahakamani.
Baada ya kudanganya mamlaka,Mayra alikiri kua mpwa wake aliuliwa na dada yake anayefahamika kwa jina la Jaime ambaye inasadikika kuwa alianza kumpiga na kitu kuanzia mida ya asubuhi siku ya tukio hilo.Dada huyo alihamia hapo na mme wake mwaka 2008 ili kumsaidia Mayra ambaye alikuwa hawezi kumlea vizuri kutokana na hali aliyokua nayo.
Mayra alisema siku ya tukio hilo la kifo dada yake alikuwa anampa chai mpwa wake huyo lakini mtoto akawa hataki kitendo kilichomkasirisha na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na alipoona amemuumiza sana,alimfunika na nguo na kumuweka pembeni mwa Mayra na yeye kuondoka.Mayra aliongeza kuwa kitendo cha dada yake kutaka kumuona mtoto wake alipopelekwa hospitali ndo kilimfanya adanganye kwani aliombwa na dada yake aseme yeye ndo ameua ili aweze kuruhusiwa kuonana na mtoto wake kwani polisi hawakutaka kuruhusu mtu yeyote hadi uchunguzi wa nani anahusika ujulikane.Hivyo Mayra hakupenda kumuona dada ake anahangaika hivyo ikabidi akubali kuhusika na kifo cha mpwa wake huyo.
Baada ya kuridhika na ushahidi huo MAHAKAMA iliamuru Jaime Rosales kutumikia miaka 15 jera kwa kosa la kumuua mwanaye.
source:daily mail
|
No comments:
Post a Comment