Saturday, July 19, 2014

18+ ONLY:FACEBOOK YAFUTA GROUP LA WANACHUO KWA KUPOST PICHA ZA UTUPU!

Uongozi wa mtandao wa kijamii Facebook umefuta group la wanachuo wanaosomea masuala ya siasa na historia wa Warwick nchini Uingereza lililojulikana kama Warwick Rowing Society baada ya kuvunja sheria ya mtandao huo kwa kupost picha za Utupu zinazotumika kutengeneza kalenda ambazo huuzwa duniani kote kwa ajili ya kupata fedha kuisaidia taasisi ya kansa ya Macmillan.
Wanachama wa jamii hiyo ya wanachuo w Warwick wakiwa katika picha ya kutangaza kalenda yao
Wanachama wa jamii hiyo ya wanachuo walionekana wamepozi utupu karibu na mashua n nyingine wakiwa wanaendesha mashua.
Wanachuo hao wakiwa wamepozi kuongeza uelewa wa kalenda yao ya kuongeza fedha kuchangia taasisi ya kansa Macmillan
Dhima ya group hilo ilikua kuongeza uelewa kwa jamii duniani kote ili kupata mauzo mazuri ya kalenda yao na kufikia malengo yao ya kusaidia taasisi y kansa ya Macmillan ambapo malengo yao ilikua kupata kiasi cha fedha cha paundi elfu tatu arobaini (3,400).
Wanachuo hao wamebakia njia panda baada ya Facebook kulifuta group lao kwa madai ya kushawishi vitendo vya ngono kutokana na picha za utupu walizokua wanapost.
 Hata hivyo Uongozi wa facebook umesema umechukua uamuzi huo baada ya kuwapa ONYO mara nyingi kutoa nbaadhi ya picha zao za utupu walizokua wanapost na imechukua uamuzi huo baada ya kuona hakuna mabadiliko kwa onyo waliyotoa kwa mwanzilishi wa group hilo.
Naye msimamizi na mwanzilishi wa group hilo Sophie Bell mwenye umri wa miaka 20 amesema Facebook haijawatendea haki kwani wanakwamisha kufikiwa kwa malengo yao ikizingatiwa wao ni wanafunzi na hawana bajeti ya kutangaza kalenda yao hiyo zaidi ya kutumia mitandao ya jamii kama facebook kutangaza kwa jamii ya watu wengi zaidi duniani.
Msimamizi na mwanzilishi wa group hilo Sophie Bell(Kulia) akiwa na wanachuo wenzake ambao ni wanachama wenzake.
Baadhi ya picha nyingine zilizofanya group hilo kufutwa na facebook.


Group hilo lina tovuti ambayo hutumika katika kuuza kalenda hizo ambapo bei hutofautiana kutokana na aina ya picha na pozi husika. 
One Media inaipongeza facebook kwa kitendo hicho kwani ni muhimu kusimamia sheria ilizojiwekea hasa katika kutunza na kuhifadhi maadili pia tunashauri vijana kutumia njia sahihi za kujitafutia kipato bila kujali malengo ya kipato hicho.

No comments:

Post a Comment