Kampuni moja ya software nchini uingereza
imekuja na app mpya inayojulikana kama mCouple kwa ajili ya kujibu maswali
mengi hasa ya Uaminifu katika ndoa mbalimbali duniani ambapo app hiyo itafanya
simu za wanandoa kufanya kazi kama moja yaani itafanya wanandoa kujua kila
kitu anachofanya mwenzi wake kwenye simu. mCuople app inauwezo wa kujua kila
kitu kinachofanyika ndani ya simu na pia kounesha mahali mtu alipo.Kwa mfano kutoa
taarifa kwa mweza wako kihusiana na calls zote zinazoingia na kutoka, ujumbe
mfupi wa maandishi, emaila pia kwa mambo yote yanayoendelea kwenye mitandao ya
kijamii kupitia account yako kama vile facebook na skype.
App hiyo imetengenezwa na kampuni moja nchini
Uingereza inayojulika kama mSpy. Uongozi wa mSpy unasema umetengeneza app hiyo
kwa ajili ya wanandoa kufanya shughli kwa amani huku wakiwa wanafahamu mwenza
wake anafanya nini kwa mda husika na yupo sehemu gani. Pia mSpy wamesema app
hiyo itawekwa kwa simu ya wanandoa kwa makubaliano ya kila mtu na isitokee
mmoja wao kuweka bila mwenzi wake kutambua kwani atakua ameenda kinyume na
dhumuni la kuanzishwa kwa app hiyo.
Hata hivyo watu wengi wanaitumia vibaya kwa
ajili ya kukamata wenzi wao ambao sio waaminifu katika mahusiano. mCouple app
haishauriwi kuwekwa kwa wenye mahusiano ambayo sio RASMI kama vile rafiki wa
kike/kiume.
Wanasheria wanasema mCouple app ni kinyume
cha sheria kwani inaingilia uhuru wa mtu hasa inapotumiwa kwa ajili ya kumpeleleza
mmoja kati ya wanandoa au wachumba.
Swala la kuhoji je ni kweli app hiyo
itatumika kama inavyotarajiwa au itasababisha matatizo makubwa kwenye familia
duniani kote!
Kwa wale wafuatiliaji wa stori za mitandaoni mnajua madhara ya app hiyo kama ilivyotokea katika ndoa ya mastaa fulani hapa bongo.
Au app hiyo inaweza kutumika kama mpango
mkakati wa kutimiza program ya Mchepuko sio diri katika nchi yetu?!!
App hiyo inatumika kwa wanandoa wanaotumia SMARTPHONES tu.
No comments:
Post a Comment