Wednesday, September 26, 2012

CHELSEA YAUA CARLING,MAN CITY HOI!

Timu ya soka ya chelsea jana ilianza vizuri mashindano yanayojulikana kama CARLING nchini Uingereza baada ya kushinda 6-0 dhidi ya Wolves.
Magoli ya chelsea yaliwekwa kimiani na wachezaji Cahill dk 4, Bertrand dk 8, Mata dk 17, Romeu (pen) dk 53, Torres  dk 58 na Moses dk 71.











Nao vijana wa Manchini, Manchester City walikubali kipigo nyumbani cha 4-2 kutoka kwa timu ya Aston Villa.Man city walikua wa kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake Super Mario kwenye dk ya 27 kabla ya Barry kujifunga katika dk ya 59 yaa mchezo na kufanya matokeo yawe sare 1-1.
Dakika ya 64,mchezaji wa man city Kolarov aliongeza bao la pili kwa city na kuongoza kwa mda kabla ya mchezaji wa aston villa Agbonlahor kusawazisha goli hilo katika dk ya 70 ya mchezo.
Hadi mpira unaisha dk ya 90 timu hizo zilikua sare ya 2-2.
Aston Villa waligeuka na kuwa mwiba mkali kwa man city katika dk za nyongeza ambapo walifanikiwa kuongeza magoli mawili kupia kwa wachezaji N'Zogbia  dk ya 96 na Agbonlahor dk ya 113.
Hadi mwisho wa mchezo huo Aston Villa 4-2 Man City.









No comments:

Post a Comment