Shindano la uchoraji kwa taasisi za elimu tanzania kwa msimu wa pili zimeanza leo baada ya wasimamizi wa shindano hilo iMage profession wakishirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) kulitangaza rasmi katika ukumbi wa habari MAELEZO uliopo dar es salaam.
wasimamizi wa shindano la uchoraji kutoka iMage profession,kuanzia kushoto ni bw.Erick Chrispin(msemaji wa shindano),bw,Fredrick Roy Manning(mratibu wa shindano) na Abdallah Chapa(mjumbe wa shindano) |
Mratibu wa shindano hilo bwana Fredrick Roy Manning kuwaambia waandishi kuwa shindano la mwaka huu litakua na ujumbe wa 'sanaa hufuatisha maisha' au 'art imitates life' ambapo washiriki wanatakiwa kuchora mchoro wowote wakizingatia ujumbe huo.
mratibu wa shindano bwana Fredrick Roy Manning. |
Naye msemaji wa shindano bwana Crispian alisema kwamba shindano limeanza rasmi leo na mwisho wa kupokea michoro hiyo itakua tarehe 30 mwezi wa disemba mwaka huu.
Waandishi walipata fursa ya kuuliza maswali kwa wasimamizi wa shindano hilo ambayo yalijibiwa ipasavyo na timu nzima ya image profession.Pia mjumbe wa shindano kutoka image profession ndugu Abdallah Chapa aliwaonesha waandishi baadhi ya michoro iliyoshindishwa mwaka jana lililokua na ujumbe wa 'kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania'
.
iMage profession inashirikiana na BASATA katika huo mradi ambapo iliwakilishwa na bwana Pastori John ambapo aliwaomba waandishi watumie pen zao vizuri kulifikisha ipasavyo shindano kwa jamii,naye mgeni mualikwa katika mkutano huo ambaye ni msanii mashughuli katika fani ya sanaa za uchoraji mzee Raza aliiomba Serikali kuweka mkazo katika fani ya uchoraji kwa kuanzisha somo husika katika shule hasa za msingi.
Mr.Raza kushoto akiongea jambo na mwakilishi kutoka BASATA Mr.Pastor John wajat |
Uongozi wa iMage profession pia uliomba utokezaji wa WADHAMINI katika shindano hilo la kipekee ambalo linahusisha watu wa rika mbalimbali inayofanaya kuwa eneo nzuri la uwekezaji.
Shindano hilo linatarajiwa kufikia tamati mwakani mwezi wa nne(4) ambapo washiriki 3 kutoka katika kila kundi watapewa zawadi.
Makundi ya shindano hilo ni kama ifuatayo;a)SHULE ZA CHEKECHEA,b) SHULE ZA MSINGI,c)SHULE ZA SEKONDARI na la mwisho ni kutoka TAASISI ZA ELIMU YA JUU NA VYUO MBALIMBALI.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kupitia anuani zifuatazo;
DRAWING COMPETITION
IMAGE PROFESSION
P.O BOX 92
DAR ES SALAAM
simu no.+255 222 644 740/+255714 676217/+255713 484040.
email:info@imageprofession.com. Ama kuwakilisha michoro katika ofisi yao iliyopo opposite na NMB Bank Msasani.
No comments:
Post a Comment