Tuesday, October 16, 2012

CHRISTIANO RONALDO KUINGIA KWENYE ORODHA MPYA!!

Mshambuliaji wa timu ta Real Madrid na Portugal,Christiano Ronaldo ataingia kwenye orodha mpya ya wachezaji ambao wametumikia timu zao za taifa kwa michezo 100 ya kimataifa akiwa na umri chini ya miaka 30.
Christiano aliingia kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Kazakhstan mwezi wa nane(august),2003 akiwa na umri wa miaka 18 tu.
Christiano Ronaldo akipewa ushauri na mchezaji mwenzake Helder Postiga kabla ya kuingia kuitumikia timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza 2003.
Ronaldo alipokua anaitumikia timu yake kwa mara ya kwanza 2003.

 Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 atatimiza michezo 100 na timu yake ya taifa watakapokua wanacheza na timu ya Ireland kaskazini mjini Oporto.
Ronaldo akijiandaa na mechi ya jumanne wiki hii.
 Kuna wachezaji wengi duniani wanaokaribia 200 ambao wametumikia timu zao za taifa kwa zaidi ya mara 100 ila wapo juu ya miaka 30 kigezo kinachowatoa kwenye orodha hii.

Wachezaji wengine ambao wapo katika orodha hiyo ya kutumikia timu zao za taifa kwa mara 100 wakiwa na umri wa chini ya miaka 30 ni hawa wafuatao.

LUKAS PODOLSKI(UJERUMANI)
Alitimiza michezo 100 akiwa na umri wa miaka 27 kwenye timu yake ya taifa kwenye michuano ya Ulaya mwaka huu dhidi ya Denmark katika hatua ya makundi.Podolski alianza kuitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya Ulaya mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19.
Podolski akishangilia goli baada ya kufunga wakati akiitumikia timu yake ya taifa kwa mara ya 100 dhidi ya Denmark.



FERNANDO TORRES (HISPANIA)
Torres alitimiza michezo 100 walipocheza mechi ya kirafiki na Saudi Arabia akiwa na miaka 28 mwaka huu.Mshambuliaji huyo alianza kutumikia timu yake ya taifa mwaka 2003.
Torres alipotimiza michezo 100 dhidi ya Saudi Arabia.


LONDON DONOVAN(AMERIKA)
Mchezaji mashughuli wa taifa la Amerika ambaye alitimiza michezo 100 akiwa na umri wa miaka 26 dhidi ya timu ya Argentina ambapo walitoka sare butu.
London Donovan wa Amerika akiwa uwanjani akitimiza michezo 100 dhidi ya Argentina.

RIGOBERT SONG(CAMEROON)
Beki huyo wa kimataifa wa Cameroon anapatikana kwenye orodha hii baada ya kufikisha michezo 100 mwaka 2006 dhidi ya Angola kwenye kombe huru la mataifa ya Afrika.
Rigobert Song akimiliki mpira dhidi ya mchezaji wa Angola kwenye kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 2006.

IKER CASILLAS(HISPANIA) 
Alitimiza michezo 100 mwaka 2009 dhidi ya Argentina.
Iker Casillas alitimiza michezo 100 mwaka 2009 baada ya kuanza kuitumikia taifa lake kuanzia mwaka 2002 kama kipa namba 1 wa taifa hilo,

No comments:

Post a Comment