Wednesday, October 3, 2012

J-LO AFUNIKA PARIS AKIWA NA WATOTO WAKE PAMOJA NA 'SERENGETI BOY' WAKE.

Msanii maarufu nchini Marekani Jennifer Lopez(43) ambaye ni mama wa watoto mapacha(Max na Emme) jumanne ya wiki hii alifanya shopping akiwa pamoja na watoto wake bila kumsahau 'serengeti boy' wake Casper Smart(25) kwenye jiji la paris Ufaransa.
J-LO akiwa pamoja na boyfriend wake Smart.
Katika shopping hiyo ambayo ilijaa wapiga picha wa vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia familia hiyo.
Smart na J-LO wakiwa wamemshika mkono Emme huku msaidizi wao akiwa amembeba Max.


 Mahusiano ya kimapenzi kati ya Jennifer Lopez na Casper Smart yamekuja baada ya mwanamama J-LO kutengana na mume wake ambaye walikuwa wote na kufanikiwa kupata watoto hao mapacha wenye miaka 4 hadi sasa.
Wapenzi hao wameonekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja wakifurahia maisha ambapo kuna wakati J-LO alisema anahamu ya kupata watoto wengine na boyfriend wake huyo.



J-LO akiwa amemshika mtoto wake Emme akiwa na mchumba wake Smart.
Kutokana na kigezo cha umri cha wapenzi hao,inasemekana familia ya Jennifer Lopez hawafurahii mahusiano hayo kwani wanaona kama ni ya mpito tu japo Smart amewahi kuwaambia marafiki zake kua anampenda sana mwanamama huyo japo amezidiwa umri.
Kuna uvumi pa Smart alimfanyia vituko mchumba wake wa zamani hadi wakaachana na ndipo haikuchukua mda kwa yeye kuwa na mwanamama Jennifer.
Baadhi ya picha za wapenzi hao nyingine ni hizi hapa.






       Jennifer Lopez aliachana na mumewe nguli wa muziki Marc Anthony mwaka mmoja uliopita.
=Marc Anthony akiwa na Jennifer Lopez enzi hizo wakiwa pamoja.

No comments:

Post a Comment