Wednesday, October 3, 2012

YANGA,SIMBA HAKUNA MBABE.

Watani wa jadi wa soka la Tanzania timu za Yanga na Simba zimetoka sare ya goli 1-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa.

Simba ilikua ya kwanza kupata goli kupitia mchezaji wake Amri Kiemba katika dakika ya 4 ya mchezo goli lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinaisha.
Yanga ilirudisha goli hilo kwa mkwaju wa penati uliopigwa kiufundi na mshambuliaji wa timu hiyo Said Bahanuzi katika kipindi cha pili dk 65 ya mchezo.

Katika mchezo huo ilishuhudia mchezaji wa Yanga Simon Musava akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kucheza faulo huku akiwa na kadi ya njano kitendo kilichoifanya apewe kadi nyingine ya njano na kufikisha jumla ya kadi 2 ya njano na hivyo kutolewa nje ya uwanja.
Pia katika mchezo huo ilishuhudia mchezaji Kelvin Yondani  akitoka baada ya kuchezewa rafu mbaya na Haruna Moshi Boban 'Balotelli wa tz',
Yanga iliingia uwanjani ikiwa na rekodii mbaya ya kufungwa mabao 5-0 katika mchezo wa mwisho walipokutana.
Hadi refa anapuliza filimbi ya mwisho timu hizo zilikua zimetoshana nguvu.


                                   kwa picha zaidi endelea kufuatilia!!

No comments:

Post a Comment