Thursday, October 4, 2012

OBAMA AVURUNDA MBELE YA MPINZANI WAKE KATIKA MDAHALO WA URAIS MAREKANI.

Raisi kipenzi cha Wamarekani Barack Obama jana alishindwa kuonesha ukali wake kwenye nyanja ya siasa baada ya kuonesha udhaifu wa hoja mbele ya mpinzani wake kutoka chama cha Republican bwana Mitt Romney wakati wa mdahalo wa kwanza wa kugombania uraisi.

Wamarekani wengi pamoja na vyombo vya habari vilitaja mdahalo huo kama JANGA kwa raisi Obama kwani umempunguzia sifa mbele za Wamarekani na kumpandisha mpinzani wake Romney.
Pia wengine walisikika kuwa Raisi Obama alikua 'nje ya mchezo' katika mdahalo huo huko mpinzani wake Romney aking'ara ipasavyo.
Bwana Romney alimfananikisha Raisi Barack Obama kama watoto wake kitabia enzi za utoto wao ambapo mpinzani huyo alisema ana watoto wa kiume wa tano,aliendelea  'watu wengi hukataa kitu ambacho si cha kweli ila unapozidi kukiongea ndipo kitageuka kua ukweli na kuaminiwa'.
Matt Romney akisisitiza jambo wakati wa mdahalo huo.
Naye shabiki mkubwa wa raisi Obama bwana Andrew Sullivan aliliambia jarida moja baada ya mdahalo huo kwamba raisi Obama amefanya vibaya hasa upande wa kujieleza,kuzungukazunguka wakati wa kujibu hoja na kukosa kujiamini.
Katika mdahalo huo raisi Obama alionekana anauchovu/kachoka huku kama hayuko kwenye hali ya furaha.
Mpinzani wa Obama alikuwa bega kwa bega na mkewe ambapo kabla ya mdahalo huo walikuwa wamekaa pamoja kusubiri muda uanze kama wanavyoonekana.
Obama alipingwa sana na bwana Romney hasa katika sera zake za uchumi ambapo mpinzani huyo ambaye pia ni msomi wa biashara amemwambia raisi Obama amefanya vibaya katika kipindi alichokuwepo madarakani ambapo uchumi wa nchi hiyo tajiri duniani umeshuka.
Wakati wa mdahalo huo bwana Matt Romney kutoka Republic alionekana mtu mwenye kujiamini kitendo kilichomfanya hata mke wake awe ana amani na furaha mda wote.
raisi Obama akijibu hoja mbele ya mpinzani wake Mitt Romney.

mke wa Mitt Romney,Ann Romney akiwa mwenye furaha wakati wa mdahalo huo.
Baadhi ya picha za matukio wakati wa mdahalo huo wa jana usiku ni kama zifuatazo




msafara wa magari wa raisi Obama ulipokua unawasili kwenye sehemu ya mdahalo.
Hata hivyo baada ya kumalizika kwa mdahalo huo wake wa wapinzani hao walikumbatiana kwa upendo huku mwanamama Ann akionyesha furaha isiyo na kifani.

Mke wa raisi Obama hakushindwa kumfariji mme wake baada ya mdahalo huo kwa kumkumbati..
Haya ni maoni ya Wamarekani yaliyokusanywa na kituo cha CNN kuhusiana na nani alifanya vizuri katika mdahalo huo baina ya raisi Obama na Mitt Romney.

 Haya ni maelezo mafupi ya bwana Mitt Romney ambaye anatokea chama cha upinzani cha Republic.
Mitt Romney
Dark-haired man with graying hair at the temples, dressed in dark suit, at a nighttime indoor event
70th Governor of Massachusetts
In office
January 2, 2003 – January 4, 2007
Lieutenant Kerry Healey
Preceded by Jane Swift (Acting)
Succeeded by Deval Patrick
Personal details
Born Willard Mitt Romney
March 12, 1947 (age 65)
Detroit, Michigan, U.S.
Political party Republican
Spouse(s) Ann Romney (m. 1969)
Children Taggart (b. 1970)
Matthew (b. 1971)
Joshua (b. 1975)
Benjamin (b. 1978)
Craig (b. 1981)
Residence Belmont, Massachusetts
Wolfeboro, New Hampshire
San Diego, California
Alma mater Brigham Young University (BA)
Harvard University (MBA, JD)
Profession Management consultant, Venture capitalist, Private equity
Religion The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (Mormon)
Positions Co-founder and CEO, Bain Capital (1984–2002)
CEO, Bain & Company (1991–1992)
CEO, 2002 Winter Olympics Organizing Committee (1999–2002)
Signature Signature "Mitt Romney", first name more legible than last name
Website MittRomney.com

No comments:

Post a Comment