Tuesday, October 9, 2012

MWANA MFALME NA MKEWE WAFUNGUA KITUO CHA MICHEZO UINGEREZA.

Mwana mfalme wa Uingereza Prince William pamoja na mke wake Kate Middleton wamefungua kituo cha michezo cha timu za taifa za Uingereza.Kituo hicho kitatumiwa na timu zote za taifa hilo kutokana na kuwa na vifaa mbalimbali vya michezo yote.Jina la kituo hicho kinajulikana kama St.George's park.
St.George's Park.
Kituo hicho ambacho kina ukubwa wa hekari 330 ambacho hadi kukamilika kwake kimegharimu kiasi cha Euro 100 milioni kitakua kati ya vituo vikubwa vya michezo duniani.
Mwana mfalme na mke wake huyo walipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na wachezaji wa timu yao ya taifa ambao wanajiandaa na mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia ijumaa hii.


Kituo hicho cha michezo kinatarajiwa kutumiwa na timu za taifa hilo kwa maandalizi pia kama kituo cha kufundishia waamuzi wa michezo mbalimbali hivyo kitakua zaidi ya chuo.
Mwana mfalme alipata pia fursa ya kuongea na wachezajia ambapo alionekana akiongea na mchezaji wa chelsea Ashley Cole hasa kutokana na adhabu aliyopewa na chama cha soka cha uingereza baada ya kutumia lugha chafu kwa chama hiko kutokana na adhabu aliyopewa aliyekua nahodha wa timu hiyo John Terry kwenye mtandao wa twitter ambapo mwana mfalme alimtania kua asipokua makini chama hicho kitaifunga akaunti yake hiyo aliyotumia kutoa kauli chafu.
Familia hiyo kifalme pia ilipata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali za mazoezi katika kituo hicho ghali na cha kuvutia duniani.

Pia waliingia kwenye bwawa la kuogea wachezaji ambapo waliwakuta wachezaji wakiwa wanaoga kitendo kilichomfanya mke wa mwana mfalme kukaa mbali nao.

Baadhi ya picha zingine ya tukio hilo la ufunguzi rasmi wa kituo hicho cha St.George's Park.




                                                   Picha zingime za eneo hilo



No comments:

Post a Comment