Wednesday, October 10, 2012

KISA NA MKASA:MAKAHABA MAPACHA WAKONGWE ZAIDI, AMSTERDAM.

Makahaba hawa wameangaziwa kufuatia kutolewa kwa kumbukumbu zao na Filamu inayohusu maisha yao. Filamu hiyo, (Meet the Fokkens), inawaangazia Makahaba mapacha wenye umri wa miaka 70 Louise na Martine Fokken ambao walitufichulia siri yao katika kufanya ukahaba katika Mji maarufu zaidi kwa ufuska duniani.

 Louise na Martine hutumia muda wao mwingi wakiwa kwenye Maskani yao ya vyumba viwili katika eneo la Ijmuiden, magharibi mwa Amsterdam. Huku wakiwa wamevalia viatu vya ndala, wao huranda randa hapa na pale chumbani wakinywa kahawa na kula keki wakionekana kukosa muelekeo.

 Martine anaimba kwa sauti ya chini huku Louise akielezea masaibu yaliyoikumba familia yake na kumlazimu kukimbilia usalama wakati wa Vita vya pili vya Dunia.

 Mama yao alikuwa na usuli wa Kiyahudi, jambo walilofanya kuwa siri kubwa kwa Wanajeshi wa Nazi waliokuwa wanashika doria nchini Uholanzi. Wimbo wa Louise uligusia Furaha na Huzuni za maisha.


"Tulikuwa watoto wadogo wakati huo wa vita. Ving'ora vilipoanza kulia, mama yetu alituficha katika eneo la chini ya nyumba. hatukuwa na kofia za chuma, hivyo basi tulitumia vikaango vya kupikia kukinga vichwa vyetu. Tulionekana kuchekesha na kana kwamba tunafurahia hali hiyo."

Mapacha hao wanasema kutolewa kwa kumbukumbu zao kumebadilisha muelekeo wao; hapo mbeleni walitusiwa, sasa wanaheshimiwa "Oh ni kicheko, bila shaka ni kicheko. huna budi kucheka hata unapokuwa na huzuni kwa sbabu ni maisha yako na huwezi kuyabadilisha, lakini ni bora ukiwa unatabasamu kila mara."
Dada hao wawili wanatingisa vichwa vya ishara ya kuafikiana katika wanayoeleza.



Hata hivyo, tabasamu lao la kujilazimisha haliepuki kudhihirisha huzuni inayojitokeza machoni mwao.
"Bila shaka hatukuwaza kamwe tulipokuwa na umri wa miaka 14 au 15 kwamba siku moja tungejiingiza kwenye Ukahaba. Tulikuwa wabunifu na tulikuwa na Matarajio maishani" akadokeza Martine says.
Louise naye akaongezea: "kila siku mimi husema ni mume wangu aliyenipiga na kuniingiza kwenye ukahaba. Alikuwa mtu anayetumia mabavu na kutishia kutengana nami endapo ningekataa kufanya ukahaba ili kutafuta pesa.
"Yeye alikuwa kipenzi maishani mwangu…" akasema.
Wanawe Louise' hatimaye wakaishia kulelewa kwenye makao ya watoto. Alituonyesha mojawapo ya picha zilizopo kwenye rafu ya vifaa vya kale, inayodhihirisha nyuso zao zenye tabasamu.
Uzoefu wa miaka mingi
Martine bado anafanya Ukahaba. Anasema malipo ay uzeeni anayopata kutoka kwa Serikali ya Uholanzi hayamtoshelezi kujikimu kimaishai. Isitoshe anaugua ugonjwa wa Baridi yabisi.
 Martine anasema ijapokuwa angependa kustaafu lakini hawezi kuendelea kujikimu kimaisha. Filamu inayomuhusu inamuonyesha akiwa kazini, amejipachika kwenye kiti akiwa amevalia soksi ndefu, mshipi na viatu vya kisigino.


Martine Fokken ni kivutio kwa wanaume wakongwe badala ya vijana wanaompita bila hata kumtazama na kumkejeli kuwa amezeeka mno. Kama kawaida yake, anaangua kicheko na kusema hajali kamwe.
Anasema nyakati zimebadilika: "Vijana wa sasa ni tofauti, wanakunywa pombe sana, wamenona na hawakuheshimu. Wanapaswa kuwa kwenye pikipiki zao kama wavulana wa Kidachi badala ya kupoteza wakati wakinywa pombe."
Licha ya ushindani mkali kutoka kwa Vidosho wenye umri mdogo katika eneo la karibu, Martine hakosi wateja.
Anaonekana kuwavutia zaidi Wanaume wazee. Yeye hutumia vitu wanavyopendelea kuvaa ili kuwavutia kama vile kuingia kwenye madanguro akiwa na mjeledi huku amevaa viatu vya kisigino kirefu.
Nini maoni yako kuhusu kisa hiki?


                                                                             habari na picha zote kutoka bbc swahili.

No comments:

Post a Comment