Monday, October 15, 2012

YAYA TOURE:NILIHISI KABLA YA MECHI KAMA TUNGEFANYIWA VURUGU NA MASHABIKI WA SENEGAL

Kiungo wa timu ya Manchester City ya  ligi kuu Uingereza na pia raia wa Ivory Coast Yaya Toure amesema kua alihisi kabla ya mechi hiyo kama kungetokea vurugu kitendo kilichofanya hata kumkataza mmoja kati ya kaka zake ambaye alitaka aingie uwanjani kuangalia mtanange huo jumamosi iliyopita katika uwanja wa Stade Leopold Senghor nchini Senegali.
yaya Toure akiwa kati ya maaskari wakimtoa nje wa uwanja jumamosi hii baada ya mchezo dhidi ya Senegali kukatishwa kutokana na vurugu za mashabiki.
 Katika mchezo huo ambao ni kwa ajili ya kufuzu kucheza kombe la mataifa huru Afrika ilishuhudia vurugu kutoka kwa mashabiki baada ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba kufunga bao kwa mkwaju wa penati iliyolalamikiwa na mashabiki hao wakidai haikuwa haki katika dakika ya 70 ya mchezo.
Awali mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea aliifungia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 51 ya mchezo.
Hadi refa anakatiza mchezo kwenye dakika 72 kutokana na kusheheni kwa vurugu hizo senegali walikua nyuma kwa mabao 2-0(6-2 jumla).
Baadhi ya picha za tukio hilo la jumamosi ni kama zifuatazo.
Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba akitolewa nje ya uwanja chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Beki wa timu ya Ivory Coast Kolo Toure akiwa kati ya  polisi akitolewa nje ya wanja baada ya kukatishwa kwa mechi hiyo.

Wachezaji wakitolewa nje na polisi.

 Hivi ndivyo ilivyokua pande wa mashabiki waliokuwepo kwenye mechi hiyo baada ya kukatishwa kwa mpira.



 kwa sasa linasubiriwa shilikisho la soka la Afrika CAF kutoa maamuzi dhidi ya vurugu hizo.

No comments:

Post a Comment