Tuesday, May 24, 2016

ALEXIS SANCHEZ KUVAA JEZI NAMBA MPYA MSIMU UJAO WA 2016/17.

Mchezaji hodari wa timu ya Arsenal raia wa Chile Alexis Sanchez ambaye alikua anavaa jezi namba 17 msimu ulioisha, atavaa jezi namba 7 iliyokua inavalia na kiungo anayeondoka arsenal Thomas Rosicky.
Alexis Sanchez akiwa kwenye muonekano wa jezi mpya za msimu ujao wa 2016/17 ambapo atakua anavaa jezi namba 17.
Hii imetokea baada ya timu ya Arsenal kuonesha mashabiki wake jezi mpya za msimu ujao zitakazovaliwa uwanja wa nyumbani. Jezi hizo hazina tofauti sana upande wa rangi kwani bado rangi nyekundu na nyeupe zimeendelea kutumika. Kubadilika kwa namba ya jezi ya Sanchez kutalazimisha mashabiki wake kununua jezi mpya.
Sanchez akiwa katika moja ya mchezo msimu ulioisha akiwa na jezi namba 17.
Akiongea wakati wa kutambulisha jezi hizo mpya za msimu ujao kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema upya wa jezi hizo utasaidia katika kuongeza hamasa kwa wachezaji na mashabiki kufanya vizuri msimu ujao kwa kuchukua ubingwa ambao waliuchezea msimu ulioisha uliobebwa na Leicester city. Pia Wenger alisema mashabiki wategemee mabadiliko mengine ya namba za jezi kwa baadhi ya wachezaji msimu ujao.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za wachezaji wa Arsenal wakiwa katika jezi mpya.

Mesut Ozil

Hector Bellerin

Oliver Giroud

Carzola, Giroud na Bellerin


No comments:

Post a Comment