Mshambuliaji wa timu ya Paris Saint-German raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic aliiwezesha timu yake ya taifa kuifunga wapinzani wao Uingereza katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kufuata ratiba ya shirikisho la soka duniani(FIFA) kwa ushindi wa 4-2.
|
Mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic |
Ibrahimovic alifunga magoli yote kwa upande wa Swedeni huku D anny Welbeck na Steven Caulker wakiipatia Uingereza mabao ya kufuta machozi.
Sweden walikua wa kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Zlatan Ibrahimovic katika dakika ya 20 ya mchezo.
|
Kipa wa Uingereza Hart akishuhudia goli la kwanza lililofungwa na Ibrahimovic. |
Goli hilo halikudumu sana kabla ya mshambuliaji wa Uingereza na timu ya Manchester United Danny Welbeck kuisawazishia timu yake katika dakika ya 35.
|
Welbeck akifunga goli kutokana na mpira wa klosi uliopigwa na Ashley Young na kuisawazishia timu yake ya Uingereza. |
|
Danny Welbeck akishangilia goli |
Uingereza hawakuishia hapo baada ya kuongeza goli lingine la pili katika dakika ya 38 kupitia kwa mchezaji Steven Caulker.
|
Mchezai wa Uingereza Caulker akiifungia timu yake goli la pili katika mchezo huo. |
|
Wachezaji wa Uingereza wakishangila pamoja baada ya kufungwa kwa goli la pili |
Baada ya kua mbele kwa zaidi ya dakika 39 baada ya goli la pili,Uingereza walikubali magoli matatu ya haraka katika dakika za mwisho za mchezo huo yaliyofungwa na Ibrahimovic kwenye dakika 77,84 na 90.
|
Ibrahimovic akishangilia goli la pili alilofunga katika dakika ya 77 ya mchezo. |
|
Ibrahimovic akifunga goli lake la tatu katika mchezo huo kwa mpira wa adhabu. |
Ibrahimovic alizidi kua mwiba kwa Uingereza baada ya kufunga goli la 4 ambalo lilikua gumzo na bora kutokea kati ya magoli katika mchezo wa soka duniani kutokana na uzembe uliofanywa na kipa wa Uingereza Joe Hart.
Katika mchezo huo ambao ulikua ni 100 kwa nahodha wa timu ya Uingereza Steven Gerrard na kuufanya kua wa kumbukumbu mbaya kwa nahodha huyo anayekipiga kwenye klabu ya Liverpool.
|
Nahodha wa Uingereza Steven Gerrard akiingia uwanjani kukamilisha mchezo wa 100 ambao uliharibiwa na Ibrahimovic. |
|
Wachezaji wa Sweden wakishangilia moja kati ya magoli yaliyofungwa na Ibrahimovic. |
Hivi ndivyo vikosi vya timu hizo
Sweden: Isaksson,
Lustig (Sana 73), Granqvist (Antonsson 73), Jonas Olsson, Martin Olsson
(Safari 46), Larsson (Jansson 85), Elm, Kallstrom (Svensson 61),
Kacaniklic, Ibrahimovic, Ranegie (Wernbloom 89).
mfungaji:Ibrahimovic 20, 77, 84, 90.
Uingereza:
Hart, Johnson (Jenkinson 74), Caulker (Shawcross 74), Cahill, Baines,
Cleverley (Wilshere 61), Gerrard (Huddlestone 74), Osman, Young
(Sturridge 61), Sterling (Zaha 85), Welbeck.
wafungaji: Welbeck 35, Caulker 38.
No comments:
Post a Comment