Saturday, November 10, 2012

MKURUGENZI MKUU WA BBC AJIUZULU.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la BBC, George Entwistle, amejiuzulu.
Aliyekua mkurugenzi wa shirika la habari la Uingereza BBC,bwana George Entwistle ambaye amejiuzulu kutokana na kashfa.
Amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.
Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto.
Jeremy Paxman ambaye ndiye aliyetangaza kipindi hicho cha Newsnight kilichosababisha mgurugenzi wa BBC kujiuzulu


Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.
Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchunguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile.
 Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya".
Mkurugenzi wa BBC alipotangaza rasmi kujiuzulu kutokana na kashfa ya udhalilishwaji wa watoto.
Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma".
"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika"
Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten
 "Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amehiari kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika - uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi".
Mkurugenzi wa BBC ambaye amejiuzulu akihojiwa LIVE leo asubuhi kwenye kipindi.



                                                                                                                   source;bbc swahili.

No comments:

Post a Comment