Sunday, July 20, 2014

mCouple KIBOKO YA MCHEPUKO SIO DILI



Kampuni moja ya software nchini uingereza imekuja na app mpya inayojulikana kama mCouple kwa ajili ya kujibu maswali mengi hasa ya Uaminifu katika ndoa mbalimbali duniani ambapo app hiyo itafanya simu za wanandoa kufanya kazi kama moja yaani itafanya wanandoa kujua kila kitu anachofanya mwenzi wake kwenye simu. mCuople app inauwezo wa kujua kila kitu kinachofanyika ndani ya simu na pia kounesha mahali mtu alipo.Kwa mfano kutoa taarifa kwa mweza wako kihusiana na calls zote zinazoingia na kutoka, ujumbe mfupi wa maandishi, emaila pia kwa mambo yote yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kupitia account yako kama vile facebook na skype.

App hiyo imetengenezwa na kampuni moja nchini Uingereza inayojulika kama mSpy. Uongozi wa mSpy unasema umetengeneza app hiyo kwa ajili ya wanandoa kufanya shughli kwa amani huku wakiwa wanafahamu mwenza wake anafanya nini kwa mda husika na yupo sehemu gani. Pia mSpy wamesema app hiyo itawekwa kwa simu ya wanandoa kwa makubaliano ya kila mtu na isitokee mmoja wao kuweka bila mwenzi wake kutambua kwani atakua ameenda kinyume na dhumuni la kuanzishwa kwa app hiyo.
Hata hivyo watu wengi wanaitumia vibaya kwa ajili ya kukamata wenzi wao ambao sio waaminifu katika mahusiano. mCouple app haishauriwi kuwekwa kwa wenye mahusiano ambayo sio RASMI kama vile rafiki wa kike/kiume.
Wanasheria wanasema mCouple app ni kinyume cha sheria kwani inaingilia uhuru wa mtu hasa inapotumiwa kwa ajili ya kumpeleleza mmoja kati ya wanandoa au wachumba.
Swala la kuhoji je ni kweli app hiyo itatumika kama inavyotarajiwa au itasababisha matatizo makubwa kwenye familia duniani kote!
Kwa wale wafuatiliaji wa stori za mitandaoni mnajua madhara ya app hiyo kama ilivyotokea katika ndoa ya mastaa fulani hapa bongo.
 


Au app hiyo inaweza kutumika kama mpango mkakati wa kutimiza program ya Mchepuko sio diri katika nchi yetu?!!
 App hiyo inatumika kwa wanandoa wanaotumia SMARTPHONES tu.

No comments:

Post a Comment