Monday, July 21, 2014

KWA MARA NYINGINE: MTOTO WA MIAKA 9 AFUNGA NDOA TENA NA BIBI WA MIAKA 62.



Kwa mara nyingine dunia inashuhudia maajabu baada ya mtoto wa miaka 9, Sanele Masilela kufungu ndoa kwa mara ya pili na mke wake mwenye umri wa miaka 62. Ndoa ya sasa ilikua ya kimila kwa dhumuni la kuifanya ndoa hiyo kua rasmi.
Bwana na Bibi Sanele wakiwa katika pozi baada ya kufunga ndoa ya pili kijijini kwa Sanele.

Ndoa ya kimila hiyo imefanyika kijijini kwa bwana harusi mototo Sanele nchini Afrika Kusini. Wanakijiji wa eneo hilo walionekana kushangaa na kusema maneno mbalimbali ikiwemo kuhisi kwao kwa kudidimia na kupotea kwa maadili duniani.Ila kwa wanafamilia pande zote walionekana wenye furaha na amani kufuatia kwa tendo hilo rasmi la kimila kuidhinisha ndoa ya wawili hao.
Sanele na mke wake wakati wa ndoa hiyo ya pili ya kimila

Ndoa hiyo ilifungwa mbele ya aliyekua mme wa bibi huyo Bwana Alfred(66) pamoja na watoto wake 5 ambao miaka yao imeanzia 28 hadi 38. Bwana Alfred alisema yeye na watoto wake wana furaha kwani hawaoni tatizo la aliyekua mke wake kuolewa na mvulana na wala hajali maneno ya watu 
Aliyekua mme wa Bi. Helen Bwana Alfred akishuhudia ndoa ya kwanza ya mme mwenza  Sanele
Wakihojiwa wanafamilia akiwemo mama wa mototo Sanele ambaye anmiaka 47 alisema wao hawajali maneno ya watu, wanafanya kama iwapendavyo wao na alidai hiyo ndoa ipo kiibada na sio kisheria.

Bwana Harusi(mtoto) Sanele alifikia uamuzi huo wa kumuoa bibi Helen baada ya kuambiwa na mizimu ya mababu zake aoe mwanake akiwa motto alipokua ndotoni na bila kufanya hivyo ingewezekana familia yao kupata misukosuko mingi hivyo amefanya kitendo hicho kwa ajili ya kuifurahisha mizimu na sio uamuzi wake yeye mwenyewe. Mtoto huyo ambaye bado ni mwanafunzi alisema mda muafaka utafika kwa yeye kuoa mwanamke anayeendana kiumri na kuzaa nae watoto.
Maharusi hao wakibusiana wakati wa ndoa yao ya mara ya kwanza.
Kwa upande wake bibi harusi Helen alisema yeye anafuraha sana kwani anajiona mwenye bahati kwa mtoto Sanele kumchagua yeye awe mke wake ili kufurahisha mizimu kitendo ambacho kimepewa ushirikiano na familia yake yote huku akisema anaimani siku itafika mme wake kupata mwanamke ambaye atazaa nae kwani ndoa yao ni kwa ajili ya kufurahisha mizimu tu, aliongeza wao kama wanaigiza tu.

Bwana na Bibi Sanele wamefunga ndoa ya pili ya kimila huku katika ndoa zote hawajasaini vyeti vya ndoa na kila mtu anakaa nyumbani kwake.

                                            AMA KWELI DUNIA INA MAMBO!!!!  

No comments:

Post a Comment